Full Lyrics
REFRAIN
Kilindi cha moyo wangu kimejaa maneno ya kushukuru
Ashukuriwe Mwenyezi anayeketi katika patakatifu
Usiku mchana mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wake
Ni Mungu aketiye juu anayenilinda
Midomo yangu itaimba maneno ya kushukuru
Asante nakushukuru Bwana wa mbingu
SHAIRI 1
Anayewalisha ndege wa angani
Ndiye anayeshusha neema
Anashusha kwa viumbe vyote
SHAIRI 2
Jua na mwezi nazo nyota za angani
Ndiye aliyeziratibisha
Akanipa zawadi ya maisha